GET /api/v0.1/hansard/entries/1230704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230704,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230704/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii nimuulize swali Waziri wa Usalama wa Ndani. Nampa kongole kwa kuweza kuchaguliwa kama Waziri. Ninamshukuru pia kwa kutii amri baada ya kuitwa mbele ya Bunge hili. Ninatoka Kaunti ya Kwale na mimi ni Mama Kaunti. Swali langu kwa Waziri ni kwamba kule Kwale, nina shida ambayo imeibuka ya vijana wanaojiita ‘‘vijana wa vipanga”. Hawa ni vijana wadogo sana wa miaka takriban 13-17. Wanauana wenyewe kwa wenyewe. Wanatumia madawa ya kulevya ambayo yanazua msisimko fulani ndani ya mwili - msisimko unaomtuma kijana kwenda kumuua mwenzake. Wanaweza kuwa wamekaa mahali pamoja wakinywa kahawa lakini wakageukiana na kukatana mapanga. Nina idadi ya vijana wengi ambao wameuana kutoka mtaa mmoja hadi mwingine. Katika sehemu ya Ngombeni, kata ya Waa, mahali ambapo nilizaliwa, tuna vijiji takriban 27 lakini kijana hawezi kutoka kijiji kimoja hadi kingine iwe ni kwa kutembea au kwenye bodaboda. Hii ni kwa hofu ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. Polisi wetu wameshindwa kudhibiti hali hiyo…"
}