GET /api/v0.1/hansard/entries/1230837/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230837,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230837/?format=api",
    "text_counter": 422,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii ya kubuni Baraza la Madawa ya Kiafrika. Kwa muda mrefu, tumebebwa visivyo na wenzetu wa asili ya kizungu. Wametufanya tifikirie kwamba dawa zao ni bora kuliko dawa za Kiafrika. Ninavyo fahamu ni kwamba, wazungu wana utaalamu wa kubuni magonjwa, lakini hawana utaalamu wa kuyatibu magonjwa hayo. Nikirudi nyuma ya chanzo cha upungufu wa kinga mwilini yaani HIV na AIDS; kirusi hiki kilibuniwa kwenye maabara na kisha kikawekwa kwa wanyama. Hatimaye kiliwafikia wafungwa na kutapakaa dunia nzima. Walijaribu kukidhibiti lakini hawakuweza. Hivi leo naweza kusimama na kusema kuwa ndani ya Africa na Kenya, tunaweza kukidhibiti kirusi kinacho sababisha upungufu wa kinga mwilini. Vile vile, wazungu waliona hivyo havitoshi na wakaanza kuleta maswala ya saratani. Hivi leo, ukimwambia mtu anaugua saratani, moja kwa moja utakuwa umemmaliza. Utakuwa umemuua kwa sababu atazama katika mawazo na aanze kuhesabu miezi sita aende kupumzika futi sita chini ya ardhi. Lakini sivyo! Saratani ni ugojwa ambao unatibika na madawa yapo. Kile ambacho kinahitajika kwa hakika ni kuwa tusitiwe uoga na tupate nafasi… Natumai Mhe. Pukose atalizingatia zaidi na kuona kwamba tunafaulu kuwa na baraza letu la madawa hapa nchini Kenya. Hilo litatusaidia zaidi kwa maana kuna wengi wanaofanya utafiti hapa na pale wa kuhakikisha kwamba hayo magonjwa sugu yanatibika. Wakati mwingi wametuletea hizo mashine zao za kuzungusha damu na kutenganisha maji na damu kwa ugonjwa kama wa figo. Lakini si lazima kuwe hivyo. Dawa ziko. Hata kama figo iko na mawe, dawa za kiasili ziko. Dawa hizi zinaweza kuyeyusha hayo mawe ndani ya figo na mtu akarudiwa na hali yake ya kawaida. Dawa ziko za kufufua figo ambayo utendaji kazi umefifia au umepungua. Dawa za kuifufua hiyo figo ziko, figo ikarudia hali ya kawaida na watu wakaishi maisha ambayo si yale ya kusukumwa na mashine. Si salama tukitumia mashine sana. Wagonjwa wanaotumia mashine sana hawatapitisha miezi minane wakishaanza kutumia mashine. Hii ni kama wataishi zaidi. Sasa unakuta ile figo inasaidiwa kufanya kazi. Lakini kadri inavyosaidiwa kufanya kazi, ndivyo inavyozidi kudhoofika; ilhali dawa za kuifufua figo na iendelee vizuri ziko. Kwa hivyo, ninaunga mkono hali hii ili tuipitishe na tuwe na baraza letu la madawa. Tunafaa kukagua hata hayo ya kizungu yakija ili kuona kwamba yanaenda sawa na vile tunavyohitaji katika nchi za Afrika. Ni wakati wa Afrika kuamka na kusema hata sisi ni wataalamu katika uwanja huu wa madawa. Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa nafasi hio."
}