GET /api/v0.1/hansard/entries/1230899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230899,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230899/?format=api",
    "text_counter": 27,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kinyume na utaratibu wa asili; tukisikitika kwamba kumekuwa na ongezeko la mahusiano ya jinsia moja nchini Kenya kutokana na usambazaji wa vitabu na machapisho yanazokuza upotovu huo; tukitambua kwamba uchapishaji na usambazaji wa nyenzo zinazohusu mahusiano ya jinsia moja katika machapisho na vyombo vya habari una athari kali kwa maadili ya jamii kuhusu mwelekeo wa kijinsia; tukimaizi kwamba kuna haja ya kutekeleza sheria ili kulinda na kuhifadhi maadili ya mahusiano ya jinsia tofauti katika taifa; tukifahamu kwamba hakuna uwezekano wa kuzaa kutokana na mahusiano na ndoa za jinsia moja; tukihofia kwamba kuongezeka kwa mahusiano na ndoa za jinsia moja kunaitia jamii ya wanadamu nchini katika hatari ya kutoweka; Bunge hili hivyo basi linaazimia kwamba Serikali ipige marufuku mara moja uzungumziaji, uchapishaji na usambazaji wa taarifa zinazokuza mahusiano ya jinsia moja nchini na kuweka mikakati ya kudhibiti maudhui hayo kwa mujibu wa Ibara ya 45(2) ya Katiba na Kifungu cha 162 cha Sheria ya Adhabu ili kuikinga jamii, hasa watoto na vijana, dhidi ya kufikiwa na mielekeo potovu ya mapenzi na ndoa ya jinsia moja."
}