GET /api/v0.1/hansard/entries/1230947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230947,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230947/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Naibu Spika kwa kunipa fursa hii ya kuzungumza kwa niaba ya watu wa Malindi. Kwanza ni kumshukuru dadangu, Jane Kagiri, kwa Hoja hii ambayo ameileta hapa. Hoja hii imeletwa hapa wakati mwafaka kwa sababu Wakenya wengi wanalalamika kuhusu jinsi gharama ya maisha iliivyopanda juu. Ninatoka katika sehemu za Malindi, ambapo tunategemea sana masuala ya utalii. Inanisikitisha leo hii ninapozunguka Malindi na kuona hoteli nyingi zimefungwa. Ukiwauliza hao wawekezaji ni kwa nini wamefunga hoteli hizo, bei ya stima huwa ni sababu kubwa. Nina imani kuwa imekuwa shida kufanya biashara katika Kenya nzima kwa sababu ya bei ya stima. Ukiangalia bei ya stima nchini ikilinganishwa na bei ya stima katika nchi za Uganda, Rwanda na Bara la Afrika nzima, utaona kuwa bei ya stima hapa Kenya iko juu, na imewakimbiza watu wasije kufanya biashara hapa nchini. Watu wanakimbilia nchi jirani ili kufanya biashara."
}