GET /api/v0.1/hansard/entries/1230953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230953,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230953/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": "za shilingi mia tano. Hili ni jambo lingine ambalo ni lazima tuliangalie sisi kama Wabunge na Serikali jinsi tutaweza kusaidia watu wetu. Katika ile shilingi mia tano niliyoilipa kununua stima, ni shilingi mia moja na themanini na nane pekee yake ndio ilitumika kununua tokens . Nilipata token s ishirini na nne peke yake. Ina maana kwamba shilingi mia tatu na kumi na mbili zinaenda kwa gharama ya malipo ambayo sielewi hadi sasa. Katika ile shilingi mia tatu na kumi na mbili, tunajua kuna ushuru ambayo ni shilingi hamsini na nane na nukta moja sita. Fuel Energy Levy ilichukua shilingi mia moja na sabini na tano; Forex Charge ikachukua shilingi arobaini na saba, ilhali malipo ya Energy andPetroleum Regulatory Authority (EPRA) ikachukua shilingi 0.73; Water Resources Authority (WRA) ama Mamlaka ya Rasilimali za Maji shilingi 0.26, na Inflation Adjustment ama Marekebisho ya Mfumko wa Bei ikachukua shilingi 20.76. Hii inamaanisha kuwa ikiwa uwezo wa mama mboga pale chini ni shilingi mia tano kila wiki, basi anaponunua tokens, haitakuwa ya shilingi mia tano. Shilingi mia moja na themanini na nane peke yake ndiyo itatumika kununua tokens . Shilingi mia tatu na kumi na mbili zinaenda kwa matumizi tofauti tofauti ambayo hatujajua umuhimu wao kama Wakenya. Ningependa kuwaeleza viongozi wenzangu kuwa hivi sasa tunapambana na hali ngumu katika nchi yetu ya Kenya. Ni sharti tuweke vichwa pamoja ili tuangalie jinsi tunaweza kunasua watu wetu kutoka katika shida wanazopambana nazo. Kwa hayo machache, ninamuunga mkono dada yangu, Mhe. Jane. Hivi leo umeweza kuleta Hoja hii, lakini isimalizike hapa. Kama tatizo ni watu wa KP, basi ni lazima tuwafuate na tuwaulize ili watueleze ni kwa nini tuko na shida kama hizi. Hatufurahii hali hii na tunataka tulete mabadiliko. Asante sana Mhe. Naibu wa Spika."
}