GET /api/v0.1/hansard/entries/1231025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1231025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231025/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Bw. Spika wa Muda. Nampongeza Mhe. Mathenge kwa kuleta Hoja hii leo. Kwa hakika, kamari imekuwa donda sugu katika Taifa hili. Wahenga walisema samaki mkunje angali mbichi. Watoto wetu wameharibika na hata nyumbani inabidi kina mama wafiche vipochi vyao. Watoto wa shule wanazama wanapoona na kusikiza michezo hii kwenye vyombo vya habari na mitandaoni. Kama Waisilamu, Qur’ani imekataza na kuharamisha kamari. Na chochote ambacho kimemchukiza na kukataliwa na Mwenyezi Mungu, binadamu anapojihusihsa nacho, basi madhara yanayofuatia huwa ni makubwa sana. Namshukuru Mhe. Mathenge kwa sababu ameona na kufichua kuwa kamari ina madhara mengi kuliko faida katika jamii. Vyombo vya habari, kuna mambo mengi mazuri mnayotueleza na kutufunza sana. Lakini tunawaomba muweze kupinga jambo hili la kamari. Kuanzia asubuhi hadi saa sita usiku, vyombo vya habari huonyesha mambo haya ya kamari. Wazee wanaoheshimika wamezama kwenye michezo hii ya kamari kufikia kuuza mashamba yao na watoto wanabaki bila urithi. Utapata wanawake wengi sana wamekaa pembeni wakishiriki katika michezo hii. Huu ni wizi wa dhahiri kutoka kwa sekta hii, kwa sababu hao wanatengeza mamilioni lakini Wakenya wanaolengwa na michezo hii ni wanyonge na hali yao ni duni. Wengine wanaenda mjengo na wakiwekeza na kushinda Ksh200, wanaendelea kuongeza pesa ili washinde zaidi. Mwingine akipata Ksh10,000 katika mjengo, anawekeza zote kwenye kamari na mwishowe anajitia kitanzi kwa sababu hali si hali. Kama kiongozi katika Jumba hili, ingekuwa ni uwezo wangu, ningepinga kamari kabisa katika Taifa hili ili tusiwe na mambo ya kamari kabisa, kwa watoto au kwa watu wazima. Sote tunaadhirika. Ingekuwa ni uwezo wangu, ningekataa michezo ya kamari. Mimi kama Mama Zamzam na Mwisilamu nakataa kamari kwa sababu dini yangu imeikataa. Nawaomba viongozi walio hapa pia waikatae kamari. Kuna mambo mengi sana tunaweza kufanya ili kulijenga Taifa. Mvua imenyesha na pesa hizi zinazotumika katika kamari ziwekwe kwenye kilimo. Tulime mashamba ili tuvune chakula. Wananchi wanakufa kwa njaa. Tuwekeze pesa hizi kwa vitu vya maana na tuwache mambo ambayo yamelaaniwa na Mwenyezi Mungu. Wazazi pia waangalie watoto wa shule. Tusiwape watoto wadogo simu, kwani tunapowapatia simu, wanaingia kwenye sites ambazo zinawaonyesha mambo ya kamari na mwishowe wanaingilia wizi. Tunawapoteza watoto wetu lakini kwanza tunapaswa kutibu chanzo cha mambo haya. Wizi huanza na mambo ya kamari, na mwishowe mtu anabadilika kuwa jambazi sugu. Kama kuna Wizara inayohusika na maswala ya kamari, basi inafanya hivyo kinyume na sheria. Wizara hii inapaswa kuangalia ni wapi kamari inachezwa – katika casino, nyumbani ama kwenye vyombo vya habari. Hata mimi nilicheza kamari nikiwa mdogo, lakini naomba Mwenyezi Mungu anisamehe. Jambo hili huanza pole pole, na mwishowe kuwa kama addiction. Watoto hushindwa kusoma na kupotea njia na tunapata jamii inaangamia. Mimi naeleza Serikali kuwa wakati mwingine inaweza kuona inakusanya ushuru hapa na pale na kumbe inachukua laana ikiiweka katika taifa letu. Ikiwa Mwenyezi Mungu amekataa kamari, basi ni dhahiri shahiri kuwa Serikali pia inaweza kupinga kamari. Sisi"
}