GET /api/v0.1/hansard/entries/1231027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231027,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231027/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "tunasema Serikali ipinge kamari kabisa ili hizo pesa zipelekwe kwa maendeleo. Nafuatilia sana. Kuna watoto ndani ya Mombasa County wameingia katika kamari. Badala ya kwenda skuli, unawapata wamekaa vichochoroni. Mkoba uko mgongoni lakini yuko na simu. Wazazi wangu wa Mombasa County, janga hili la kamari ni janga kubwa, ijapokuwa halionekani. Leo mtoto atakuletea mia tano akuambie: “Maa, mimi napata hizi. Ninabeti, napata hizi tununue mboga”. Wewe mama unapokea lakini jua unaweka mtoto wako katika matatizo. Kesho atafungua kabati lako na kutoa dhahabu zako aende kuuza ili apate pesa za kucheza kamari. Kesho kutwa atafungua mlango wa jirani, ataangalia kipochi chake na kuchukua akacheze kamari. Siku inayofuata ataenda kuvunja benki. Utampata kwenye casino. Wale wa kuvunja benki wakishamaliza shughuli zao huenda katika casino kutupa pesa kama njugu maanake hawakuzifanyia kazi. Hawajui uchungu wa pesa. Yote yanatokana na mambo ya kamari. Kwa hivyo, Mheshimiwa Spika wa Muda, leo ninafurahi kupata mwanya huu wa kupinga kamari kabisa na kuunga mkono mjadala wa Mhe. Mathenge. Mheshimiwa, Mwenyezi Mungu akuweke. Huu ni mijadala wa nguvu sana katika Jumba hili; ni kati ya mijadala mikubwa sana katika taifa hili; ni donda sugu ambalo lilikuwa limefumbiwa jicho. Leo tunaliangazia. Nina uhakika ninyi Waheshimiwa wenzangu mtaweza kulitilia maanani na kupinga haya mambo ya kamari, hasa katika mateleshiveni yetu. Mnaotangaza ni wazazi - mna watoto. Tunawaomba tuanze kutoa mambo ya kamari katika vyombo vya habari kisha tuimalishe sehemu nyingine yoyote ile. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda."
}