GET /api/v0.1/hansard/entries/1231268/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1231268,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231268/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Swali hili alilouliza ndugu yetu, Sen. Wambua, ni swali muhimu kwa wakati huu. Tunaelewa ya kwamba huu ni wakati mgumu sana kiuchumi. Pia, Serikali yetu imekuwa na shida ya kuweza kulipa madeni yake ya nje na madeni mengine tofauti na hata mishahara ya wafanyikazi. Hilo ni jambo ambalo linajulikana sana. Swali hili ni muhimu kwa sababu linataka kujua ni pesa ngapi ambazo shirika hili la KRA limeweza kukusanya katika kipidi hicho. Tumeona wamekuwa wakigeuza viongozi pale juu lakini mpaka sasa hatujui ni pesa ngapi zilitolewa kuweza kulipa madeni? Swala lingine ni kwamba, katika muhula huu wa uchumi ambao umepita, ni hatua gani Serikali inachukua kuona ya kwamba madeni yake yamefanyiwa mipango ya kuilipa ama taratibu za kuweza kulipa? Badala ya suala hili kuchunguzwa na Serikali, ni muhimu pia sisi wananchi kujua jinsi kodi tunazolipa zinatumika. Tunafaa kujua kama wanatumia kulipa madeni na mishahara. Kufikia sasa, madaktari na wafanyikazi wengine wa Serikali hawalipwa mishahara yao. Watalipwa lini mishahara yao?"
}