GET /api/v0.1/hansard/entries/1231562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231562,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231562/?format=api",
"text_counter": 416,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii, kuchangia Muswada wa ugawaji wa fedha baina ya Serikali kuu na Serikali za ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, kwanza kabisa, napinga Mswada huu kama ulivyoletwa katika Bunge hii. Mswada huu unasema kwamba, pesa ambazo zitatoka katika Serikali kuu na kuja kwa serikali za kaunti ni shilingi 385.425 bilioni. Ukiangilia hii shilingi 370 bilioni ni zile zilizotolewa mwaka wa 2022/2023. Kwa hivyo, hakuna chochote ambacho kimeongezeka, isipokuwa shilingi 15 bilioni, ambazo wamesema ni mapato waliyoyafanyia marekebisho. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia swala la mlipuko wa bei za bidhaa, kwa mfano, mafuta; mwaka jana mwezi wa saba, bei ya mafuta ilikuwa ni shilingi 125 kwa lita. Hivi leo, mafuta ni shilingi 174 kwa lita ambalo, ongezeko la karibu asilimia 40. Hiyo pekee inaonyesha kwamba gharama za utoaji huduma katika kaunti zetu imeongezeka mara dufu, kiasi ambacho haiwezekani kutoa huduma kwa fedha zile zilizotolewa mwaka uliopita. Bw. Spika wa Muda, kwa hivyo, ongezeko la shilingi 15 bilioni katika pesa ambazo zitakwenda katika kaunti zetu ni kidogo sana ukilinganisha na ongezeko ya mapato ya Serikali, kama ilivyo katika table ya pili ya Mswada huu. Mapato ya mwaka wa 2023/2024 yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya shilingi 430 bilioni. Lakini, kaunti zimepewa shilingi 15 bilioni peke yake ya fedha hizo. Bw. Spika wa Muda, jambo la pili ambalo ningependa kuguzia ni kwamba Hazina Kuu au National Treasury haiwezi kuwa huru, wakati kiongozi wa Hazina hii ni Waziri wa Serikali kuu. Ninavyosema ni kwamba, haiwezekani awe yuko na uhuru ya kugawa fedha bila ya kupendelea upande wowote ikiwa tayari yeye yuko upande wa Serikali kuu. Bw. Spika wa Muda, viongozi wa Halimashauri ya kukusanya Ushuru, ama"
}