GET /api/v0.1/hansard/entries/1231566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231566,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231566/?format=api",
"text_counter": 420,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wanateuliwa na Waziri wa Serikali kuu. Kwa hivyo, Hazina Kuu haijakuwa huru kama vile ilivyotarajiwa na Katiba yetu ya 2010. Iwapo Hazina Kuu itakuwa huru, basi itakuwa ndio nafasi mwafaka ya kugawa fedha kisawasawa, baina ya Serikali hizi mbili za ugatuzi na Serikali kuu. Bw. Spika wa Muda, vile vile, ipo haja ya kuifanya ile ofisi kuu ya madeni iwe huru kutoka kwa Wizara ya Fedha ya Kenya. Hii inamaanisha, watakuwa na nafasi ya kutoa ushauri ambao ni huru kwa Serikali kuu, kutokana vile wanavyokopa pesa kiholela holel, ili kudhibiti fedha za Serikali."
}