GET /api/v0.1/hansard/entries/1231568/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231568,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231568/?format=api",
"text_counter": 422,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, jambo la tatu ni kwamba, kuna huduma ambazo serikali zetu za ugatuzi hutoa. Kwa mfano, huduma ya kilimo imetolewa kutoka kwa Serikali Kuu ambayo inatakikana itoe mwongozo wa vile ambavyo wanafaa wafanye. Lakini, tumeona hivi majuzi, Serikali Kuu inaingilia maswala ya kununua mbolea na kupeleka katika kaunti. Serikali Kuu inaenda mpaka nchi za nje kutafuta mashamba ya kulima mahindi wakati wakulima wetu wanashindwa kulima kwa sababu ya mkurupuko wa bei za bidhaa, ikiwemo mbolea na maswala kama hayo. Pesa zile bado zinalala katika Serikali Kuu zitoke ziende kwa serikali za ugatuzi ili bajeti zetu za maswala ya kilimo, uvuvi na maswala ya kuendelesha Serikali na kuwapa chakula wananchi katika nchi yetu, ziweze kupata huduma hizo kwa urahisi na watoe bidhaa bora za kutuendeleza. Bw. Spika wa Muda, haiwezekani sisi tutakuze kilimo Zambia wakati hapa tuna Galana-Kulalu, Bura na Mwea ambazo bado hazijakamilika. Pia sehemu zingine ukulima unaendelea katika nchi yetu. Vile vile, kwa maswala ya afya, tumeona madaktari wakilalamika kwamba maslahi yao bado hayajafuatiliwa. Sen (Dr.) Khalwale yuko hapa na nasikitika hakuligusia swala hili wakati alipokuwa akiunga mkono Mswada huu. Maswala ya madaktari na huduma za afya ni muhimu sana. Tusipoangalia madaktari vizuri, huduma duni zitaendelea kutolewa katika zahanati na hospitali zetu. Watu wengi watagonjeka na mwishowe kupoteza maisha yao. Maswala ya Managed Equipment Scheme (MES) hayakutajwa hapa. Lakini hii MES ilisaidia pakubwa kupeleka vifaa vya kisasa katika hospitali nyingi, ambapo vifaa vile havingefika. Hili swala lazima liangaliwe tena upya kwa sababu tunaona vifaa bado vinahitajika na hospitali zinapanuka."
}