GET /api/v0.1/hansard/entries/1231580/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231580,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231580/?format=api",
"text_counter": 434,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ", kumetolewa Kshs425 milioni. Pesa hizi ni kidogo sana. Haziwezi kutosha zile kaunti kumi na tatu zilizopangiwa kupata pesa hizo kutokana na huduma za maktaba. Mswada huu pia umeeleza kwamba mara nyingi, ni Serikali Kuu ambayo inapata pigo iwapo pesa zilizonuiliwa kukusanywa hazitakusanywa zote kwa mwaka unaohusika. Lakini, kwa muda wa karibu miaki miwili, Kenya Revenue Authority (KRA) inayokusanya ushuru kwa niaba ya Serikali Kuu imepitisha kiwango ambacho walitarajiwa kukusanya. Hiyo inamaanisha kwamba zile pesa za ziada ambazo zimepatikana huwa zinatumika katika Serikali Kuu peke yake. Hazipelekwi kwa serikali za kaunti kama inavyotarajiwa. Si kweli kwamba Serikali inapata hasara wakati makadirio ya pesa hayataweza kufikiwa. Chochote kinachopatikana lazima kigawanywe sawasawa kulingana na dharia kwamba serikali zote mbili zinatoa huduma kwa wananchi katika Jamhuri ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, kwa hayo mengi, ninapinga Mswada huu."
}