HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231600,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231600/?format=api",
"text_counter": 454,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ninaunga mkono Mswada huu wa ugavi wa mapato. Kwanza, nitajadili suala la maabara. Ningetaka kumkosoa Seneta wa Tana River, Sen. Mungatana, na kumwambia kuwa si kaunti za kaskazini peke yake ambazo hazina maabara. Katika zile kaunti hazina maabara, ya kwanza ni Kirinyaga, Busia, Homa Bay, Kajiado, Lamu, Machakos, Nyamira, Samburu, Tana River, Tharaka Nithi, Trans Nzoia, Turkana, Vihiga na West Pokot. Kaunti ambazo zimenyanyaswa na kuachwa nyuma kwa muda mrefu pia zinapewa nafasi katika hii Hazina ya Usawazishaji yaani, Equalisation Fund. Wale ambao hawana maabara ndio wangekuwa wanapewa zile fedha kwanza kuhakikisha wamejenga maabara katika kaunti zao. Ni kwa nini kaunti ambazo hazina maabara zimeachwa bila kuwa na maabara na hili jambo halitiliwi maanani? Ni kusema katika sehemu zile hawana akili na hawataki kusoma? Wakati tunasema hizi pesa, Ksh425 milioni, zinaenda kwa kaunti zile ziko na maabara peke yake, zile hazina, kwa nini zisiangaliwe kwanza ziwe na maabara? Ni zipi ziko sawa, zile ziko na maabara ama zile hazina? Mtoto mwenye mwenye njaa ndiye unampa chakula kwanza na aliyekula jana angojee kidogo ili huyu ale ndio waende wakiwa sawasawa. Ningeomba wakati hizi pesa zinagawanywa kwa muhula ambao unakuja, iangaliwe na kuhakikisha kwamba kila kaunti imepewa pesa zake, ijipange pia kujenga maabara. Pili, ni kweli tunakaa hapa mpaka usiku kujaribu kupata pesa ambazo tunatuma katika zile kaunti tulizotoka. Hata hivyo, unapouliza maswali kuhusu vile zile pesa zinavyotumika, wakati mwingine, Wawakilishi Wadi wanatumwa wakutusi wakisema hufanyi kazi yako. Hapa, wakati tunaenda mawindoni, sijasikia gavana anatutusi kwa sababu tunasema apewe pesa. Nimejiuliza maswali mengi. Kwa mfano, gavana anaenda katika Kamati ambayo inahusika na kufuatilia hesabu ya pesa zilizotumika katika kaunti, akiitishwa stakabadhi na Seneti akose kuzileta, kwa nini pia aje agawiwe pesa? Kwa nini tusiweke sheria ya kwamba awasilishe stakabadhi na kama pesa zimepotea, kwanza arudishe ndipo agawiwe pesa zingine? Tunavyoendelea kuwagawia hao watu pesa na maswali hatuulizi, ndivyo wanaendelea kuwa vichwa ngumu. Wengine wako na vichwa ngumu kuliko karai ya kupika chapati. Ukiwauliza maswali, ndipo unajipata katika shida usizoweza kuelezea. Katika idara zilizotajwa, naona kuna National Treasury, CoG, CRA, ICPAK, IPP na Institute of Economic Affairs. Kwa nini Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali,"
}