GET /api/v0.1/hansard/entries/1231606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1231606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231606/?format=api",
    "text_counter": 460,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nashukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia Mswada ambao umeletwa hapa. Cha msingi ni kutarajia kwamba hizi fedha tunazoachilia kuenda mashinani, tusiwe kama wale ambao wanafanya katika maeneo ya kuhifadhi waliofariki, kwamba tunafanya upasuaji wa fedha za serikali. Tunataka chini ya uongozi wako, Seneti hii, iwapo kazi ni nyingi na ni mzigo kwa walio katika Kamati hiyo, tuweze kupewa nafasi wengine wetu tuweze kutia msasa vitabu vya hesabu vya kaunti mbalimbali. Isiwe kwamba wako nyuma kwa miaka miwili au mitatu. Tuweke magavana hao kwenye mizani na tuwapige msasa ili tufuatilie kama fedha walizopata zinafanya kazi au la. Bw. Spika wa Muda, ninaomba tu, kwa uongozi wako, tupewe hiyo kazi na tuifanye kabisa."
}