GET /api/v0.1/hansard/entries/1231815/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1231815,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231815/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Leader of Minority",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Spika, hili Bunge la Seneti ni Bunge la heshima na tunajiheshimu tukiwa hapa. Hatuna ubaguzi. Huku kuna waheshimiwa ambao wamevaa kwa hali ya heshima zaidi na upande huu vile vile. Lakini tukiangalia upande huu, kuna doa moja ambalo ni bwana mwenyekiti wangu, ninamheshimu, ni kijana mdogo vile vile kama Sen. Methu. Sijui hii tabia wameanza lini. Vile vile, kichapo kile kile alichokula Sen. Methu, ni kichapo kile kile ambacho ndugu yangu, Sen. Thang’wa - ambaye ni rafiki yangu mkubwa na ninamheshimu sana - anapaswa kukula pia. Anafaa kuvaa kama Sen. Wakili Sigei, ndugu yangu Kiranja wa Walio wengi Bungeni, Sen. Mandago na avae kama mimi kama kielelezo tunayowaonyesha. Bw. Spika, tunataka uamuzi wako tafadhali."
}