GET /api/v0.1/hansard/entries/1231842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1231842,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1231842/?format=api",
    "text_counter": 231,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bwana Spika, kwa kunielekeza. Nilileta Kauli hapa katika Seneti kuhusu kukatwa kwa nguvu za umeme katika Hospitali kuu ya Pwani yani Coast General and Referral Hospital . Niliomba Taarifa ile ninafikiri mwanzo wa mwezi wa tatu na hadi leo sijapata ripoti yoyote kuhusu mikakati ambayo Kamati imefanya ili kuchunguza na kuupata ukweli kuhusu kusisitshwa huduma katika hospitali kuu. Ni muhimu kwa sababu nguvu za umeme zinahitajika katika hospitali hususan katika vile vitengo vya wagonjwa mahututi, watoto waliozaliwa kabla ya umri wao na sehemu zingine zinazohitaji nguvu za umeme. Ningependa Mwenyekiti wa Kamati, atoe shauku kuwa hakuweka Kauli ile chini ya kiti. Asante."
}