GET /api/v0.1/hansard/entries/1232023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1232023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232023/?format=api",
"text_counter": 412,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa hii fursa ya kuchangia Mswada huu wa ugavi wa pesa za serikali kati ya Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Mwaka wa 2010, tulijipatia Katiba mpya ambayo ilileta awamu mbili za serikali; Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Katika uundaji wa zile serikali ama ile Katiba, tukaunda Tume inaitwa Commission on Revenue Allocation (CRA) ambayo kazi yake ni kusaidia katika ugavi wa pesa za Serikali. Pia Katiba yetu ikaweka Bunge mbili katika nchi hii; Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti. Hizi Bunge, zinawakilisha wananchi katika viwango tofauti. Nikiangalia huu Mswada ambao umekuja leo mbele yetu, ile tume ya ugavi wa pesa imependekeza kauti zipokee Kshs407 billion. Lakini National Treasury imependekeza serikali za ugatuzi zipokee Kshs385 billioni. Hilo ni ongezeko kutoka kwa Kshs370 billioni ambayo ilipeanwa kwa serikali za ugatuzi mwaka uliopita wa kifedha 2021/2022. Bi. Spika wa Muda, napinga huu Mswada kwa sababu tuliweka tume ya CRA sisi ya kubaini vile pesa zitakavyo gawanywa. Nawaomba Wabunge wote kutoka pande mbili; yaani Walio Wengi na Walio Wachache tushirikiane kwa kuunga mkono pendekezo la CRA kuwa Kshs407 bilioni zipelekwe katika kaunti zetu. CRA ni tume ambayo tuliweka sisi wenyewe katika Katiba yetu na vyema tuiheshimu. Wamefanya kazi yao kisayansi na ni vyema tuangalie vile vigezo walivyoweka ama walivyoangalia ili kuafikiana kuwa Kshs407 billioni uwe ni mgao wa kaunti zetu. Jambo la kwanza ambalo tume ya CRA ilibaini ni mfumuko wa bei ama ongezeko la gharama ya maisha ambayo sasa hivi ni asilimia 9.2. Kwa hivyo, naunga mkono kwamba zile pesa zitakazoenda kwa magatuzi ziwiane ama ziwe sambamba na mfumuko au ongezeko la gharama ya maisha. Nitashangaa nikiona Seneta yoyote katika Bunge hili ambaye atasema kwamba kaunti zinyimwe pesa au zipewe pesa duni. Kwa wale tulikuwa katika lile Bunge lililopita, naona hapa Sen. Wambua na wengine; tulipigana vita sana na Serikali. Kupitisha Mswada wa Division of Revenue ilituchukua miezi minne. Maseneta wengine waliwekwa ndani lakini hatukufa moyo mpaka Serikali ya Kitaifa ikakubali kupeana kwa serikali za ugatuzi Kshs370 billioni."
}