GET /api/v0.1/hansard/entries/1232025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1232025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232025/?format=api",
    "text_counter": 414,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, leo hii nawaomba Maseneta wenzangu, kwa heshima na taadhima tukubali kupeana kwa serikali za ugatuzi Kshs407 bilioni ambazo zimependekezwa na tume ya CRA. Serikali za ugatuzi zinafanya vizuri mashinani. Zimejenga hospitali, zahanati na shule nyingi. Je, tutajengaje shule bila kupeleka rasilimali za kutosha kuajiri waalimu wa shule za chekechea na kadhalika mashinani? Je, tutaajiri vipi waalimu wa vyuo vya anuwahi, madaktari na wauguzi bila kupeleka rasilmali mashinani? Kwa hivyo, kama tume ya CRA inasema tupeleke leo Kshs407 bilioni na wametumia vigezo vya kisayansi ili kufikia kiwango hiki cha pesa hatuna budi sisi ila tu kuheshimu pendekezo lake. Tukiangalia pesa ambazo Hazina ya Kitaifa inapendekeza zipelekwe katika kaunti zetu ni Kshs385 bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia nne. Kutoka Kshs370 bilioni hadi Kshs385 bilioni ni ongezeko la asilimia nne za pesa zinazoenda kwa kaunti zetu. Lakini ukiangalia katika Serikali ya Kitaifa, pesa zilizoenda ni Kshs413 bilioni. Hili ni kiwango cha asilimia 23. Kwa nini tupewe ongezeko la kaunti asilimia nne na kwa Serikali ya Kitaifa asilimia 23 zaidi? Hili ni jambo ambalo halikubaliki na katika Serikali ambayo inaongoza sasa ya ‘makalio juu’ ama Bottom Up, walisema wataangalia mtu wa chini. Kuangalia mtu wa chini ni kupeleka pesa zaidi katika serikali za ugatuzi ili mambo ya ukulima, viwanda, madawa na kujenga hospitali yaangaliwe. Lakini tukipunguzia serikali hizi za ugatuzi pesa, basi ule mfumo wa ‘makalio juu’ tutakuwa tuna uhujumu. Ni vizuri tupeleke pesa zaidi kwa magatuzi na pande zote mbili; pande ya Walio Wengi na pande ya Walio wachache tushikane mkono---"
}