GET /api/v0.1/hansard/entries/1232041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1232041,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232041/?format=api",
"text_counter": 430,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninafikiri dakika zangu zimehifadhiwa kutokana na hitilafu ya mitambo. Bunge la Seneti, chini ya Article 96 ya Katiba, liliundwa ili kulinda ugatuzi. Katiba ya kwanza ya 1964, ilikuwa na magatuzi na Bunge la Seneti. Lakini waliokuwa pale hawakuweza kulinda magatuzi. Ni jukumu la hii Seneti ya 13 na zile zijazo, kushikana mkono ili kulinda ugatuzi. Ugatuzi tunaulinda kutokana kwa nani? Unapoangalia vile kunaendelea hivi sasa, ni miezi minne tangu serikali zetu za ugatuzi zipewe pesa. Hii ni njia moja ya kuua ugatuzi hapa nchini. Njia nyingine ya kuua ugatuzi ni kupunguza zile pesa ambazo zinafaa kwenda kwa magatuzi na kupeana pesa nyingi zaidi Serikali ya kitaifa. Hii ndio njia nyingine ya kuua serikali za ugatuzi. Bi. Spika wa Muda, kuna watu waliopinga hii Katiba ya mwaka wa 2010. Sasa hivi, wao ndio wako uongozini. Waswahili husema, “mama wa kambo si mama.” Inaweza kuwa, yule mtoto ambaye wanamlea sio mtoto wao na ndio maana tunaona mambo kama haya ya kupunguza pesa za kwenda kwa serikali za ugatuzi kwa sababu, kwanza, hawakuamini hiyo Katiba. Huwezi ukalea mtoto ambaye sio wako. Bi. Spika wa Muda, ninaomba kwa heshima, tuungane mkono na Maseneta wenzangu wa upande zote mbili, ili tupeleke pesa nyingi kwa ugatuzi. Kwa hivyo, tutapendekeza Mswada huu ufanyiwe marekebisho ili tupate kuupitisha. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}