GET /api/v0.1/hansard/entries/1232206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1232206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232206/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Nashukuru sana. Mimi pia ningependa kutoa maoni yangu kwa sababu ya Seneta Mheshimiwa anayesimamia Walio Wengi katika Seneti. Kwa wale wanafunzi ambao wametoka Kericho High School ni shukrani sana. Nimeamua kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ningependa kuwauliza nyinyi kama wanafunzi muendelee kuisifu na kuitumia lugha yetu ya Kitaifa. Sababu ya hiyo ni kuwa katika Seneti, tukijadiliana na kuzungumzia maswala kuu kuhusu nchi yetu, tunatumia lugha mbili - Lugha ya Kiingereza na ya Kiswahili, haswa wale ambao ni viongozi wenu kama mhe. Cheruiyot na mhe. Cherarkey. Unajua zamani, Bw. Naibu Spika, mtu aliyetoka katika jamii ya Kalenjin, hata Rais mwenyewe, alikuwa hazungumzi lugha ya Kiswahili vizuri. Siku hizi, lugha ya Kiswahili inazungumzwa na viongozi katika jamii ya Kalenjin kwa njia safi. Wanazungumza hiyo lugha kisanifu na ni heshima kuwa wameendelea kuhimiza kuwa lugha yetu ya taifa iendelee kusifiwa na kutumika. Vile mnavyojua, mimi kama Seneta wa eneo wakilishi la Kisii County, ningependa kuwasifu na kuwapa wosia kuwa muendelee kuwa marafiki na wale vijana wetu ambao wanatoka Kisii. Hii ni kwa sababu ninajua wanafunzi wengi wametoka eneo la Kisii na wanasoma kule Kericho. Ningependa kusema kuwa, Kericho ni eneo la taifa yetu ambalo tunaliheshimu, kwa sababu ya kukuza chai na maendeleo mengine. Nikimalizia, taifa hili ni lenu. Hakikisheni katika miaka 10 au 15 ijayo, na nyinyi mje hapa muwe Maseneta, Wabunge katika Bunge la Kitaifa. Wengine watakaokuwa wahandisi na kadhalika nao waendelee kufanya kazi zingine. Asante Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi kuzungumzia hili jambo."
}