GET /api/v0.1/hansard/entries/1232273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1232273,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232273/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika. Ninapenda kuwakaribisha wanafunzi na walimu kutoka Kaunti ya Kirinyaga. Kaunti hii ni jirani ya Kaunti ya Embu. Karibu sana katika Bunge hili la Seneti ili muone ambavyo tunavyofanya . Sisi pia tulikuwa wanafunzi kama ninyi. Msome kwa bidii ili wengine wawe Maseneta na pia Rais wa nchi hii. Pili, ni aibu kubwa kuwa mmewasili leo na mkapata tukiongea kuhusu mambo ya kilimo. Katika kaunti hizi mbili mvua ilikuwa kidogo ilhali tunahitaji chakula. Hadi wakati huu, hatuko mahali pazuri. Kwa hivyo, tunaomba mkirudi katika kaunti zenu mpande miti. Tunaomba pia department zingine zitusaidie na maji ya kilimo. Nina support huo mjadala kutoka Seneta. Pia, tuafaa tuone vile tutapata chakula kingi. Sen. Mumma, ingekuwa ni mambo ya kurusha mawe, naona kuwa ungerusha. Tumewazoea. Lakini ikija ni mambo ya chakula, lazima tukubaliane. Mungu amefanya miujiza na mvua ikanyesha. Kwa hivyo, tuko tayari kupanda na kufanya kazi yote. Ninaunga mkono mjadala huo. Ingekuwa ni mawe mngerusha."
}