GET /api/v0.1/hansard/entries/1232620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1232620,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232620/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sisi kama Maseneta tumetembea sana. Mimi mwenyewe niemenda Colorado, Dubai na nchi zingine. Wakati walianza kujenga barabara zao walikuwa wamewacha sehemu kubwa sana ya barabara. Lakini hapa Kenya, wakati wa ujenzi wa barabara hatutenge sehemu hizo. Itakuwa ngumu kwetu sasa kutengeneza sehemu ya watu ya kutembelea Huku mjini huenda ikawa mambo ya ajali ya gari si mengi lakini ukienda vijijini, utakuta vijana wetu wanaendesha pikipiki bila kujali. Kwa hivyo, ningeomba Waziri aweze kuangalia kama kuna uwezekano katika kila kaunti vijana wetu wanaweza kuchunguzwa kila mwaka kama wametumia dawa za kulevya, pombe na kama akili zao ni timamu. Hii ni kwa sababu kila siku, baada ya dakika chache, hata bila gari au bila kitu chochote kinamsumbua barabarani, unakuta ameanguka na ameaga dunia. Jambo hili linapaswa kuchunguzwa na Kamati ya Seneti. Ni lazima Seneti ichukue hatua ili kusaidia vijana wetu kwa sababu vijana wetu wako hatarini. Wakati kuna ukosefu wa usalama au vita nchini, ni vijana wetu wanaweza kutupigania. Hata wasichana wetu hawatapata watu wa kuwaoa ikiwa wavulana wetu wataendelea kufa ovyo barabarani. Kwa hivyo, jambo hili linapasa kuchunguzwa kwa makini. This is a matter of emergency. Asante, Bw. Spika."
}