GET /api/v0.1/hansard/entries/1232625/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1232625,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1232625/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "barabarani hakuna hatua inayochukuliwa kwa sababu maofisa wa polisi huchua hongo kutoka kwa wenye magari ya abiria. Nasimama hapa kumuomba Waziri wa Barabara, Uchukuzi na Ujenzi, kando na matakwa ya huyu mlalamishi ya kuweka daraja ya kutumiwa na watu kuvuka barabara hiyo, kuna umuhimu kuweka ishara za barabarani. Hizi ni Road Safety Signs katika lugha ya Kingereza. Tutaendelea kunyorosha vidole kwa madereva. Wengi wa madereva wa magari ya abiria wanachangia pakubwa katika hizi ajali tunazozishuhudia barabarani zetu. Sisi kama Serikali tunapaswa kuweka ishara za barabara ili tuweze kuwaongoza madereva wetu. Pia madereva wa boda boda bali na kuyahatarisha maisha ya Wakenya wengine, wanahatarisha hata maisha yao. Nimezungumzia kuhusu hongo zinazochukuliwa barabarani na maofisa wa polisi. Mtakubaliana na mimi ya kwamba kuna vijana wengi baada ya kukosa ajira, wanapewa"
}