GET /api/v0.1/hansard/entries/1233866/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1233866,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1233866/?format=api",
    "text_counter": 355,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Dan Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Nitasema machache sana. Kwanza ninatoa pole zangu kwa familia zilizopoteza wanafunzi na mwalimu. Mimi kama mzazi, ningependa kusema kwamba Serikali ina jukumu kubwa la kuchunga watoto wetu wakiwa shuleni. Haitakuwa vyema wakati wa mitihani tunaona Mawaziri wakikimbia kila mahali wakifuatilia mitihani isiibiwe ama kufanyiwa vibaya. Lakini suala hili la afya lazima Serikali ilivalie njuga na kuangaliwa kwamba Mawaziri wanaohusika wa afya na elimu, wanatembea kwa shule zetu zote na kuangalia ni vipi wanafunzi wanaishi katika mabweni, na pia kuangalia kama wana facilities za kutosha ili janga kama hili lisitokee tena. Mhe. Spika wa Muda, nikimalizia, tumepoteza watoto wetu katika ajali za barabara na mambo tofauti. Tunakataa shetani huyu wa kupoteza watoto wakiwa shuleni. Kwa hivyo, Serikali lazima itupatie ripoti kamili. Je shule zetu ziko vipi?"
}