GET /api/v0.1/hansard/entries/123413/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 123413,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/123413/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mwenyezi Mungu amemweka hapa mwawakilishe watu wake ili mweze kusikia vilio kama hivyo lakini wengine wetu tunakipuuza kilio hicho. Mimi niliupinga Mswada wa kwanza ulioletwa Bungeni. Mhe. Imanyara, na viongozi wengine wengi, pia waliupinga Mswada huo kwa sababu ulikuwa umetayarishwa na hila. Mswada huo ulikuwa umeandikwa kuwatetea wauaji na wavunjaji sheria. Mimi na Waziri Msaidizi mwingine mmoja tu ndio tulioukataa Mswada huo miongoni mwa wale tuliomo Serikalini. Tulilazimishwa na Serikali kuunga mkono Mswada huo lakini tulikataa. Tulisema kwamba haiwezekani kwa sababu Mswada huo haukufaa. Nikauliza: âKwa nini Mswada huu hauna vipengele ambavyo vinamruhusu kila mtu kulingana na mwingine kisheria?â Lakini hakuna aliyetaka kulijibu swali hilo, isipokuwa tu kutulazimisha kuja hapa kuunga mkono Mswada huo, ambao haukuwa unafaa. Kwa hivyo, nikasema âlaâ. Ukaja mswada wa pili ambao ulikuwa na tatizo kama hilo, nikasema âlaâ. Bw. Naibu wa Spika, leo hii, kuna Mswada ambao umependekezwa kwetu na mhe. Imanyara, na ninampongeza mhe. Imanyara kwa kazi nzuri aliyofanya ya kuuandika Mswada huu vile inavyotakikana. Hakuyatoa mambo haya kutoka kwa kichwa chake, bali ameifuata sheria. Amefuata mapendekezo yaliyowekwa na kuratibishwa na viongozi wetu wakati walipoweka sahihi yale makubiliano baada ya vita. Kipengele cha Nne cha ile memoranda waliyoweka sahihi kinasema kwamba mtu yeyote atakayepelekwa kortini kwa mashtaka ya kuvunja sheria ni lazima aondoke Serikalini. Mtu huyo ni lazima aondolewe madaraka pamoja na mshahara wake na marupurupu yote anayopata kutoka kwa Serikali. Wakuu wawili wanaoshikilia Serikalii, pamoja na wale Mawaziri wengine wanane waliokuwepo, waliweka kidole wenyewe. Walisema kwamba sheria ni lazima ifuatwe na korti kuandaliwa ili haki itendeke kwa walioadhirika. Bw. Naibu wa Spika, ninashangaa kuona kwamba labda wameusahau huo mkataba waliouweka mbele ya macho ya wananchi wa Kenya. Bw. Ocampo aliwasili humu nchini kuyashughulikia mambo hayo lakini wale wazee wawili wanaoshikilia Serikali, ambao ninawaheshimu sana, walirudisha nyuso zao nyuma na kukataa kumuruhusu Bw. Ocambo kuwafungulia mashtaka wahalifu hao. Wawili hao waliogopa kusema hivyo kwa sababu miongoni mwa wale waliotenda madhambi hayo ni marafiki zao."
}