GET /api/v0.1/hansard/entries/1234144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1234144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234144/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria West, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Mathias Robi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili pia niweze kuchangia hii Ripoti ambayo imeletwa katika Bunge hili. Ripoti hii ni nzuri sana katika nchi yetu ya Kenya kwa kuwa inajali maslahi ya binadamu. Tunapozungumzia mapenzi ya kulazimisha kazini, inaonyesha tabia isiyo nzuri. Katika hii nchi ya Kenya, lazima tutilie maanani hayo maneno. Waswahili pamoja na sisi tunasema kuwa mapenzi hayalazimishwi. Kama mtu hajakubaliwa sio lazima amlazimishe mwenzake. Hili jambo limetokea kila mara. Tumeona mambo yakijitokeza na tunataka kutoa onyo kali sana. Ningependa kumpongeza yule Mheshimiwa aliyeleta Hoja ya yale matatizo yanayotokea kule Kericho. Alifanya vizuri. Kericho ni sehemu inayojulikana kwa majani chai, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}