GET /api/v0.1/hansard/entries/1234146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234146,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234146/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria West, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Mathias Robi",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, hatuwezi kusema kuwa hii hali inawapata wanawake pekee bali wanaume pia. Kuna wanawake ambao pengine wamempenda mwanaume fulani na yeye kuna uwezekano hawapendi, anaweza akalazimishwa kimapenzi. Hili jambo tunaloliongea ni la huzuni na aibu. Vile tumeumbwa humu duniani inafaa tufuate maagizo ya ngono vizuri. Kumaanisha, kama mwenzako hajakukubali, ni makosa na marufuku kumlazimisha kufanya ngono. Katika Bibilia, tunajua mwanaume na mwanamke waliumbwa, wakawekwa sehemu moja na wakaambiwa wazae ili tuongezeke. Na hayo yaweze kutimika, tunatakikana tuwe tumekubaliana kuwa wakati unamlazimisha mwanamke mlale naye unafanya makosa. Hapa Kenya, tunataka kuambia Serikiali ifuatilie sana maeneo yanayofanya mambo kama hayo. Utapata kuna yule bosi mmoja ambaye badala ya kutumia hekima, unakuta kuna msichana amemtamani na huenda alienda kwake kutafuta kazi na badala amsaidie kupata kazi ya kihakika kwa sababu amesoma, anamwambia afanye mapenzi naye ili apate kazi."
}