GET /api/v0.1/hansard/entries/1234415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234415,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234415/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Onyonka. Sheria zetu zinasema vijana na walemavu wapewe kazi. Hata hivyo, ni jambo la kuvunja moyo kuona baada ya wao kupewa kazi, hawajalipwa kwa wakati ufao. Siyo Kaunti ya Kisii pekee yake, bali kaunti nchini ambapo unapata watu wengi hawajalipwa. Wawekezaji na wafanyi kazi wengi wanasononeka sababu tayari wamechukua mikopo ya benki. Inakuwa ni vigumu sana kwao kuweza kuendelea na biashara zao ilhali kaunti hizi zaendelea kupokea pesa na kuchagua ni nani watakayelipa. Ikiwa wewe hauwaungi mkono kisiasa, haulipwi. Kamati itakayohusika na jambo hili inafaa iangazie mambo haya kwa undani na wale ambao wamefanya kazi wapate kulipwa pesa zao. Watu wakilipwa, kaunti zetu zitaendelea kunawiri kwa sababu pesa zitaenda mashinani. Kama tunavyosema sisi, watu waanzie mashinani wakipanda juu na itawezekana. Kwa hivyo, kaunti zetu ziwezi kulipa madeni ya watu ambao wamefanya kazi. Kama vile Sen. Oketch Gicheru alivyosema katika taarifa yake, watu wa bodaboda wanapaswa kuchungwa sana. Kazi ya Serikali ni kuchunga mali na maisha ya"
}