GET /api/v0.1/hansard/entries/1234420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234420/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Sen. Onyonka kutoka Kisii. Ninaunga mkono taarifa hii. Jambo la pesa ambazo hazijalipwa wale contractors na suppliers waliopeleka vitu na kufanya kazi katika kaunti, ni sugu sana kwa kila kaunti. Kama kaunti ya Machakos, tuko na hizi pending bills za kutoka 2014 hadi wa leo. Na bado hazijalipwa. Bw. Naibu Spika, ningeomba wale ambao wataangalia jambo hili waangalie kaunti zote na hata kuundwe jopo la kuchunguza ni watu wangapi hawajalipwa pesa zao katika kila kaunti. Mambo haya ya watu wa bodaboda ambayo yameletwa na Seneta mwenzetu ni muhimu sana katika kukuza uchumi wetu. Wanafanya kazi ya maana sana kwa sababu kusipokuwa na magari, wao ndio wanafanya usafiri. Wanastahili kulindwa na kuheshimika. Asante, Bw. Naibu Spika."
}