GET /api/v0.1/hansard/entries/1234432/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234432,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234432/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Mteule, Sen. Miraj. Kabla ya janga la COVID-19, mwaka wa 2020, ndege nyingi zilikuwa zinakuja Mombasa, kwa mfano, Turkish Airlines, Qatar Airways na nyingi nyinginezo zilizokuwa zikileta abiria na kufanya biashara katika Mji wa Mombasa. Bali na Jomo Kenyatta hapa Nairobi, MIA ni mojawapo ya vile viwanja vikubwa viwili ambavyo vina uwezo wa kuchukua ndege zote zinazoweza kuruka ulimwenguni. Ni masikitiko kwamba kutokana na ukosefu wa ndege hizo, biashara katika kaunti ya Mombasa na kaunti jirani imedorora kwa sababu ya ukosefu wa wageni wanaokuja kutalii kwenye fuo za bahari ya Pwani na kwingineko. Ndege nyingi zilikuwa zikija Mombasa. Tukiwa wadogo Condor, British Airway, Lufthansa na zingine nyingi zilikuwa zinashuka Mombasa na kuruka bila matatizo yoyote. Ni masikitiko kwamba serikali imeweza kulemaza biashara katika MIA ambayo ndio uwanja mkubwa kabisa mbali na Jomo Kenyatta hapa Nairobi. Ni muhimu kwamba kamati ambayo itashughulikia swala hili, ilishughulikie kwa undani zaidi ili kuona"
}