GET /api/v0.1/hansard/entries/1234450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234450/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Vile vile ikiwa ni ndege moja itapewa ruhusa ya kuzuru Mombasa, hakutakuwa na mashindano. Pia watalipisha nauli wanavyotaka. Tukikubali mashirika ya ndege mengine kuzuru na kutua kule itakuwa jambo la manufaa kwa wateja na watalii wataongezeka. Ndio maana tumetengeneza reli inayoenda Mombasa. Bw. Naibu Spika, ni vizuri hata ndege zile zingine ziwe zikitembelea pale. Jambo hili litaongeza ajira kwa vijana wetu. Utalii nchini utaimarika kwa kuwa watalii wengi watazuru Kaunti ya Mombasa kwa sababu nauli itakuwa imeongezeka. Uchumi wetu umezorota, na wananchi hawana hela. Ndege nyingi kutembelea Mombasa zitaleta ushindani kibiashara na bei zitapungua. Nimesikia Sen. Wambua akisema kuwa sina uwezo wa kuongea kuhusu ndege ---"
}