GET /api/v0.1/hansard/entries/1234745/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234745,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234745/?format=api",
"text_counter": 515,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Langu ni kukemea kile ambacho kilitendeka na kutoa masikitiko makubwa kwa watu wa Kaunti ya Kilifi na Wakenya kwa jumla. Watu wengi sana walikwenda na imechukua miaka nyingi sana. Hii ilianza mwaka wa 2017. Ninaambiwa hapa ya kwamba ilianza mwaka wa 2003. Haya yote yalikuwa yakitendeka katika nchi yetu tukiwa tuko hapa. Nchi ilikuwa kwenye utawala wa kaunti na ilikuwa na Gavana ilhali hatukuweza kujua kuwa watu wetu, familia zetu na ndugu zetu walikuwa wakienda kwenye huo msitu. Huo msitu umekula watu wengi. Ningeomba uchunguzi ufanywe kwa haraka. Pastor Mackenzie alikuwa ameshikwa kabla ya haya yote na alitolewa kwa faini Kshs10,000 peke yake. Kwa yale yote aliyofanya, alipewa faini ya Kshs10,000. Tunaomba uchunguzi ufanywe kwa haraka na tuweze kuona matokeo. Kuna watu waliofariki na familia zao zimeumia. Sijui ni"
}