GET /api/v0.1/hansard/entries/1234849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234849,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234849/?format=api",
"text_counter": 619,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bwana Spika wa Muda, naunga mkono hii Hoja ipelelezwe vizuri. Hoja ambayo tunajadili haifai kuleta urushaji wa maneno. Kuna mambo ya kisiasa na kuna mambo yanayohusu afya za watu. Haya si mambo ya Azimio la Umoja au Kenya Kwanza. Tunafaa kuketi pamoja kama Maseneta na kuonyesha nchi hii kazi ambayo tunafanya. Tunayamulika mambo ya Kaunti ya Kilifi na hatujamulika ya Kaunti ya Embu na pembe zote za nchi. Kenya ina Kaunti 47. Serikali ya Yesu Kristo tunayofuata kwa wakati huo ilikuwa na madaktari, walimu, wapishi na watoza ushuru na kila kitu. Lakini tulipofika wakati wa kupeleleza, tumeanza kujibizana. Tunatazama Kaunti ya Kilifi ilhali kuna mifano mingi kama hiyo katika nchi hii. Ninaomba upelelezi ufanywe kuhusu maneno haya na uanze kutoka kwa eneo ndogo,"
}