GET /api/v0.1/hansard/entries/1234853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1234853,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1234853/?format=api",
"text_counter": 623,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa sababu tunaanza kupigana kama haya ni mambo ya Azimio au Kenya Kwanza; mambo ya kurusha mawe au la. Tunataka kuonyesha dunia nzima jinsi Bunge hili la Seneti linavyoendelea kwa sababu haya ni mambo ya kishetani wala sio ya Mungu na yanahusu afya ya watu. Naomba upelelezi ufanywe kutoka kwa vongozi wote. Rafiki yangu, Seneta wa Kilifi alikuwa kiongozi wa kaunti hiyo kwa miaka kumi. Alikuwa anafanya kazi gani? Nimechaguliwa kama Seneta wa Embu na nimehudumu kwa muda wa miezi sita. Kila siku asubuhi na jioni lazima nijue matukio yote katika kaunti yangu. Seneta wa Kilifi ametuambia mambo mengine ambayo hatufahamu. Yafaa atuambie; kwa muda wa miaka kumi, alikuwa anafanya nini. Tufanye upelelezi na Seneta wa Kilifi atuambie jambo hili lilitukia vipi. Juzi watu walipoenda kurusha mawe alikuwa katika mstari wa mbele. Hakutuambia jambo lolote kuhusu watu wanaokufa Kilifi. Naunga Mkono hoja hii. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}