GET /api/v0.1/hansard/entries/1235842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1235842,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1235842/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninampongeza ndugu yetu, Mhe. King’ara, kwa kuleta mjadala huu. Watu wa boda boda wamechangia uchumi wa Kenya kuwa bora zaidi. Wameokoa maisha ya watu wengi kwa kuwa wepesi wa usafiri. Hawa ni vijana ambao wanatafuta ajira. Ninawapongeza watu wa boda boda wa Mombasa kwa sababu wako na nidhamu ya hali ya juu. Licha ya hayo yote, kuna umuhimu wa kupiga msasa sheria na kuhakikisha kuwa kuna sheria ya kuwawezesha kuwa katika njia iliyo sawa. Wanafaa kutengewa barabara zao ili wasipite mahali ambao magari husababisha ajali sana. Pia, wanafaa kujiandikisha ili tujue wale wanaoleta maafa na wakiibiwa tutajua kwa wepesi. Kenya inahitaji sheria katika kila sekta. Na sheria ni msumeno unaokata mbele na nyuma. Kuna wale wanaoharibia wahudumu wa boda boda sifa. Hao ndio tunafaa kupiga msasa ili kuhakikisha kuwa sheria na masharti yanatumika. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}