GET /api/v0.1/hansard/entries/1235902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1235902,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1235902/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "wagonjwa. Ukitengeneza sheria, huwa inapelekwa kwa Kamati, mnajadiliana, Wabunge wanahusishwa, na hata sisi tukitaka, tunaweza kuja huko kama marafiki wa hiyo Kamati maanake haya ni mambo yanayotuhusu na yanatutatiza kila wakati. Ningependa wagonjwa wapewe uhuru wa kwenda popote wanapotaka kutibiwa katika sheria hiyo. Kumekuwa na mtindo ambapo mgonjwa anapotaka kwenda matibabu India, anazungushwa tu. Madaktari wanamwambia aende kwa Kenya Medical PractitionersPharmacists and Dentists Union (KMPDU) ili ombi lake litiliwe sahihi. Akifika kule, wanamwambia hawawezi kutia sahihi na atafute daktari amtilie sahihi. Akienda kwa daktari, daktari anamwambia kuwa hawezi kutia sahihi kwa sababu huduma hiyo inafanyika Kenya. Hata kama huduma hiyo inafanyika Kenya, mbona mnamkataza mgonjwa kwenda kule anakoamini atapata huduma hii kwa urahisi? Gharama za matibabu kule ni rahisi. Kwa nini hapa Kenya pia matibabu yasiwe rahisi? Kama ni procedure inayofanyiwa hapa Kenya na inakugharimu Ksh300,000, ukienda huko nje, gharama yote pamoja na tikiti ya ndege haifiki hiyo Ksh300,000... Ukienda kule, unaangaliwa mwili mzima kwa gharama hiyo hiyo tu! Kwa hivyo, sheria isiwe ya kuwapa madaktari uwezo wa kuwafungia wagonjwa wanaotaka kwenda wanakoamini watapata matibabu vizuri zaidi. Sheria iwape wale wagonjwa wanaotaka huduma hapa Kenya mbinu rahisi ili wajue wakitaka referral, wanafuata njia gani. Ninaomba Mhe. Barasa kuwa sheria hii ikija mbele ya Kamati, mhakikishe kuwa kila eneo lina kamati ya kuwachunguza madaktari. Daktari akisema mama afanyiwe oparesheni ya kutolewa mtoto, ichunguzwe kama oparesheni hiyo ilifaa kabla hata ifanyike, au baada ya oparesheni kufanyika, waone kama kulikuwa na dharura ya kweli ya mama huyo kwenda kufanyiwa oparesheni. Kuwe na kamati katika kila eneo kwa sababu mambo kama haya yanatakikana kwa haraka. Ningeomba pia kuwe na kamati ya kitaifa ya kuchunguza madaktari kujua mbona daktari fulani amefanya oparesheni nyingi. Unapata kuwa kila mzazi akienda kwa daktari fulani, huyo daktari anamfanyia oparesheni. Tujue kama nchi zingine zinafanya hivyo."
}