GET /api/v0.1/hansard/entries/1235903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1235903,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1235903/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Itabidi sisi kama Bunge tujipange, na pia Ministry ijipange, kuwe na hospitali za rufaa katika kila eneo. Maanake hapa Kenya, kuna hospitali sita kubwa za Level 6. Lakini hizi Level6 hospitals zinapatikana katika eneo moja. Coast nzima hakuna Level 6 hospital hata moja. Kisha bado watu huku wanazungumzia ‘ one man, one vote, one shilling’ . Hospitali hizi zinafaa ziwe karibu na wagonjwa. Mtu anatoka Lamu kuja KNH kwa sababu hiyo ndiyo Level 6 hospital ambayo iko karibu naye. Kutoka Kiunga kufika Nairobi ni gharama ya juu. Watu wanakufa kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufika KNH. Hospitali yetu ya referral iliyo kubwa ni Coast General Hospital . Sheria hii inafaa izungumzie kupatikana kwa Level 6 hospital moja katika kila eneo."
}