GET /api/v0.1/hansard/entries/1235984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1235984,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1235984/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Mhe. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Namshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Uwiano kwa kuleta suala hili katika Bunge, tukijua kwamba katika nchi ya Sudan kuna Wakenya wengi. Kuna Chuo Kikuu cha Sudan ambacho hutoa udhamini wa masomo kwa watoto wengi sana Afrika nzima, hasa hapa Kenya. Mara ya mwisho nilipoangalia, kulikuwa na wanafunzi zaidi ya 1,000 katika chuo kikuu kinachoitwa International University of Afrika, Khartoum. Hao ni watoto ambao walipatiwa udhamini wa masomo, tiketi ya ndege, na makaazi ya bure. Ni wazi hawana uwezo wowote kujisimamia wakati janga kama hili limetokea. Hoja hii ni muhimu na ya dharura ili tuone ni vipi Serikali ya Kenya na vitengo vyote vya kidiplomasia vinavyohusika na usalama vitaweza kuwanusuru Wakenya wote walio kule wasidhurike. Sio wanafunzi pekee yao. Tusisahau kwamba saa hii tuna shida za kutosha hapa Kenya. Kuna Hoja ambayo imetolewa, ambayo itazungumziwa baadaye, ya maafa ambayo yametokea Kilifi. Itakuwa jambo la kuhuzunisha tukiwa na maafa mengine ya kiasi kikubwa katika nchi ya kigeni kama ‘Sudan Kusini’. Naomba Serikali na vitengo vyote vinavyohusika kuona kwamba hatua za haraka zinachukuliwa kuwanusuru Wakenya na suluhisho kupatikana katika ngazi za kimataifa. Wakati mapigano yanatokea, hakuna yeyote anayenufaika. Imefika wakati Bara la Afrika liwe bara la amani na si bara la vita. Serikali ichukue hatua za dharura. Nashukuru aliyeleta Hoja hii. Naunga mkono. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}