GET /api/v0.1/hansard/entries/1236167/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236167,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236167/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Naibu Spika, ninataka kukuambia wazi kwamba upetelevu wa kazi ya Serikali iliyo mamlakani imesababisha vifo kule Shakahola. Wapi serikali? Ilikua wapi? Makundi ya ujasusi yalikua wapi? Watu wakae bila chakula, wasinywe maji ilhali mzee wa kijiji yuko, mzee wa Nyumba Kumi yuko, msaidizi wa chifu yuko na chifu yuko? Wapi wajasusi wa Malindi na Magarini wakati watu waafa na kuzikwa bila wao kupeana taarifa kwa Serikali? Serikali imelegea katika utendaji kazi na ni lazima nizungumzie watu wa kwetu. Kwa nini haikujulikana watu wanakaa pale Shakahola? Hakuna taarifa mpaka watu wamekufa na kuzikwa. Leo mnatuletea Hoja, mkiwa upande wa Serikali, eti tuangalie haya. Serikali imekua wapi? Vyombo vya usalama vya Serikali viko wapi na watu wamekufa na kuzikwa? Hatuwezi kukubaliana na hii Hoja. Kuna upetelevu wa kazi. Polisi na wajasusi wanaangalia maandamano ya Mhe. Raila na wanaacha watu wakufe Shakahola. Mnashika Wabunge wa Azimio ilhali watu wanakufa Shakahola na hamjui."
}