GET /api/v0.1/hansard/entries/1236170/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236170,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236170/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": "Mnapoenda kununua mabomu ya machozi ya Azimio la Umoja-One Kenya Coalition Party, watu wanakufa. Serikali haijui watu wa Kilifi wanakufa. Inafaa ichukue hatua ili iweze kuona ni vipi. Mhe. Naibu Spika ni mwanasheria mkubwa. Mchungaji Mackenzie alishikwa lakini hakimu wa Malindi akamtoa kwa dhamana ya elfu kumi. Watoto wawili wamekufa. Serikali imepoteza mwelekeo. Watu wetu wamekufa kule Kilifi. Maiti zimefukuliwa. Kuna makaburi ya inchi mbili. Unataka kuniambia Chifu alikuwa hajui? Je, Mwanachama wa Kamati ya Utendaji ya Serikali ya Kaunti alikuwa hajui kule Magarini na Malindi? Lazima Serikali ichukuwe hatua na iwajibike kwa sababu watu wetu wamekufa. Watu wanakufaje na Serikali haijui? Naibu wa Kiongozi wa Wengi Bungeni ndiye macho ya Rais kule Kilifi lakini hajaenda kuona hizo maiti. Analeta tu Hoja hapa ndani ya Bunge. Hii ni aibu sana kwa Serikali iliyo mamlakani na tunataka watu wetu wachukue hatua. Asante, Mhe. Naibu wa Spika."
}