GET /api/v0.1/hansard/entries/1236188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236188,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236188/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Rabai, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii. Kwanza, ninamshukuru Mhe. Owen Baya kwa kuleta Hoja hii. Kwa niaba yangu na wakaazi wote wa Rabai, ninatoa rambirambi zetu kwa wakaazi wote wa Eneo Bunge la Malindi ambao wamepata maafa haya. Kufikia leo, kuna zaidi ya miili 90 ambayo imefukuliwa kutoka kwenye yale makaburi. Ninakashifu yale mauaji ambayo yamefanyika kupitia kwa Pastor Mackenzie. Dini inaturuhusu kufunga. Kitabu cha Mathayo sura ya nne katika Bibilia Takatifu kinasema kwamba Yesu Kristo alifunga kwa siku arobaini. Dini inaturuhusu tufunge. Kuna aina mbili za kufunga. Wakati ndugu zetu Waislamu wanafunga katika mwezi mtukufu wa"
}