GET /api/v0.1/hansard/entries/1236190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236190,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236190/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Rabai, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker": null,
    "content": ", wanaamkia njaa, wanashinda njaa, na ikifika jioni, wanafungua na kupata chakula. Waumini wa dini ya Kikristo, hususan Wakatoliki, wanafunga kwa kunywa maji na ikifika jioni, wanakula chakula. Niko hapa kukashifu kikamilifu dini ambayo msimamizi wake ni Mchungaji Mackenzie kwa sababu alikuwa anawaeleza waumini wake wafunge bila kula chakula chochote. Kama mmoja wa viongozi wa Pwani kutoka Kilifi, ningependa kusema kuwa ni jambo la aibu siku ya leo kuwa Mama Kaunti tuliyekuwa tunamtazamia asimame kidete na kuungana na wale wote ambao wamepata maafa haya kule Kilifi, leo hii yuko hapa kukashifu viongozi wengine. Hilo ni jambo la aibu sana. Ninaomba Serikali ije na taratibu. Makanisa yote yaorodheshwe ili kila kanisa litambulike. Ninaomba wachungaji wote wakaguliwe na wapewe vibali na Serikali ili tujue wachungaji hawa wanatumia njia na tabia gani za kuzungumza na waumini wao. Mwisho, ili kitendo kama hiki kisitokee tena katika taifa letu, ninaiuliza Serikali ihakikishe kuwa wazee wetu wa Nyumba Kumi na wazee wa mitaa wanalipwa mishahara. Ikiwa wazee wa mitaa na wa Nyumba Kumi wangekuwa wanalipwa mishahara, jambo hili lingekuwa limetatuliwa kabla kufikia pale limefika. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii."
}