GET /api/v0.1/hansard/entries/1236257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236257,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236257/?format=api",
    "text_counter": 335,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda na viongozi wenzangu, kwanza nakushukuru kwa kunipatia fursa hii kama Mbunge wa Malindi ili niweze kutoa hoja zangu kuhusiana na maswala ambayo yanakumba Eneo Bunge langu na Eneo Bunge la Magarini na Kilifi County kwa ujumla. Mwanzo ninatoa risala zangu za rambirambi kwa wale watu wote na familia zao ambao wameweza kupoteza maisha yao kwa sababu ya Pastor Paul Mackenzie ambaye ana itikadi kali ambazo sisi kama wananchi wa Kenya hatuwezi kukubali. Mhe. Spika wa Muda, ninachukua pia fursa hii ili nimshukuru ndugu yangu Mhe. Owen Baya kwa kuwa sisi sote tunatoka Kilifi na ninajua pia yeye ameumwa jinsi ambavyo watu wetu wameweza kupoteza maisha kupitia huyu Pastor Mackenzie. Kitu ambacho kinaniuma kama Mjumbe na kama mama ni ninaumwa na roho nikifikiria ni wanawake na watoto wangapi ambao wamekufa pasipo na hatia. Kuna watu ambao sasa hivi wanatamani uhai, kuna watu ambao wana kiu huko waliko wanataka kutoka huko walipo warudi hapa duniani ili waweze kuona watu wao na kuweza kuangalia familia zao. Inanisikitisha leo hii na ninapinga vikali hili jambo ambalo Pastor Mackenzie amelifanya. Katiba yetu inaturuhusu uhuru wa kuabudu lakini matatizo ni lazima tuseme pale ambapo yalipo. Kuna watu ambao wanajaribu kubadilisha na kupoteza watu kwa sababu ya uhuru wa kuabudu ulioko kwenye Katiba yetu. Si watu wa Malindi au Kilifi peke yao ambao wameathirika. Ukiangalia vizuri, kuna watu ambao wametoka kaunti za Kisii, Kisumu na Taita Taveta. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo limebeba kila Mkenya. Haya sio matatizo kwamba mtu amesoma ama hajasoma. Haya ni matatizo ambayo yanakumba Wakenya wote. Hili ni jambo la madhehebu ambayo yana misimamo mikali. Ningependa kuwakumbusha Wakenya wenzangu kuhusu dada yangu mmoja mrembo sana aliyesoma ambaye anaitwa Esther Arunga. Tulimpoteza dada mwenye vipaji sana kwa sababu ya masuala kama haya. Wakati ule, sisi kama Wakenya, tulinyamaza na hatukuchukua hatua yoyote. Hili ni jambo ambalo haliangalii dini moja. Tukumbuke mashambulizi ya Chuo Kikuu cha Garissa mwaka wa 2015 na maduka ya West Gate. Hivi vitendo vyote vilitokana pia na masuala ya msimamo mkali na itikadi kali zinazotumika kwa dini na ndio wanazidi kupoteza watu wetu."
}