GET /api/v0.1/hansard/entries/1236279/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236279,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236279/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ni kwa huzuni sana inabidi tuahirishe shughuli za kawaida za Bunge ili tuizungumzie Hoja ambayo ingezuilika, endapo sote kama Wakenya na viongozi tungekuwa tumewajibika vilivyo. Nchi ya Kenya inajivunia kuwa nchi ya kidini. Kuna wachache ambao labda watasema hawamuamini Mungu ama hawana dini, lakini wengi wana dini. Tunajua kuwa katika nchi yetu ya Kenya, Wakristo ndio wengi, kisha Waislamu na Wahindi. Imetokea wazi kuwa watu wanatumia dini na maswala ya dini vibaya. Tunamzungumzia mchungaji aliyeambia watu wafunge – ambayo ni fasting – hadi kufa. Sisi Waislamu tumemaliza siku 30 za kufunga. Funga haijui mtu. Funga ni tiba inayotibu magonjwa mengi kama ya kisukari, ya moyo na mafuta mwilini. Funga inakupatia uzima mwilini. Hivyo ndivyo ilivyo katika dini zote. Si Waislamu pekee; Wakristo pia hufunga. Lakini utapata kuwa lengo la watu hawa huwa si kuua hasa, ila ni kujitajirisha kwa haraka. Wanapata nafasi hiyo kwa sababu wengi wetu, hata viongozi, tumepoteza pesa kwa sababu ya kuwapatia pastors ama wahubiri pesa zetu ili ziongezeke kwa ghafla. Si muda mrefu uliopita ambapo kulikuwa na mchungaji mmoja aliyekuwa akiambia watu “wapande mbegu”. Yeye alikuwa haui mtu, lakini alitaka kujitajirisha. Wale wanaotoa pesa wana tamaa ya kutajirika, ilhali tunajua kuwa hakuna njia ambayo unaweza kujitajirisha haraka ikiwa hufanyi kazi ama biashara."
}