GET /api/v0.1/hansard/entries/1236280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236280,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236280/?format=api",
    "text_counter": 358,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Sasa hivi, tunazungumzia swala la Shakahola. Ndugu zangu ambao walikuwa wanalaumu Serikali kwamba Shakahola ni kijiji kidogo, pengine wangejifahamisha kwamba eneo la Shakahola in ekari 800. Ukubwa wa eneo hilo umekaribia mji mzima wa Nairobi. Kwa hivyo, si vyema kuuliza kuwa askari walikuwa wapi ukizungumzia eneo kubwa la ekari 800 ambalo ni msitu. Huyu bwana alienda pale kama mkulima na ndio maana aliweza kulinunua shamba hili na akaweka bwawa la maji ili kujificha. Kwa hivyo, haikuwa rahisi. Tusilaumiane kuwa Serikali ilipaswa kumjua huyu bwana. Tatizo ni sisi ambao tuko huku nje. Tukiambiwa kuwa kuna mhubiri ambaye anaweza kutufanya tupate fedha haraka, hapo ndipo tatizo lipo. Sidhani kuwa kuna mtu yeyote ambaye, kwa imani yake, anakubali kuwa akijiua ataenda mbinguni. Hakuna kitabu cha Kiisilamu au Bibilia ambacho kinaruhusu mtu kujiua endapo mtu ataweza kuisoma dini yake yeye mwenyewe na kujaribu kuielewa. Mara nyingi ni masuala ya ahadi, kuwa mimi nikipeleka fedha zangu pale nitaombewa niweze kupata fedha zaidi."
}