GET /api/v0.1/hansard/entries/1236289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236289,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236289/?format=api",
    "text_counter": 367,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia muda huu. Kwanza, kwa niaba ya wakazi wa Kaloleni, kwa niaba yangu na familia yangu nataka nitoe rambirambi kwa familia ambazo zimepoteza watu wao. Hili ni janga la kitaifa kwa sababu hatuwezi kupoteza watu zaidi ya tisini. Huyu Pastor Mackenzie amejulikana tangu mwaka wa 2017. Kwa nini bado ninalaumu vyombo na vitengo vya usalama? Tuko na mabalozi wa Nyumba Kumi, wazee wa mitaa na sub-chiefs ambao kila wakati hupeleka ripoti za ujasusi ili Serikali ijue kinachofanyika. Lakini kwa sababu hatujakuwa na dhamani na hao wazee wa mitaa na mabalozi wa Nyumba Kumi, ndio maana tumefika pahali tulipo. Nchi hii inatawalwa na sheria na Katiba na tunajua katika nchi yetu kuna uhuru wa kuabudu lakini sijaona kama kuna uhuru wa kuambia watu wafe ili wamuone Mungu. Tumesikia Mackenzie yuko na watoto 17 ambao wanaishi maisha ya kifahari. Yeye mwenyewe hajafungwa na hajakufa. Ni rahisi kutoa mfano kwa kitu chochote lakini ni vigumu zaidi wewe mwenyewe kuwa mfano. Angekuwa kweli anataka kuonyesha mfano bora wa watu kutokula The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}