GET /api/v0.1/hansard/entries/1236290/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236290,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236290/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "chakula ili wafe wamuone Mungu angekuwa wa kwanza kufunga na kufa. Hili ni kosa la jinai na huyu anatakikana kufunguliwa mashatka ya mauaji ya halaiki ya watu kule Uholanzi. Ni jambo la kutamausha kwamba baadhi ya hawa ambao wanajiita mapastor wameona njia ya kujitajirisha ni kufungua makanisa. Ni jambo ambalo baada ya kujitajirisha, wao hutumia pesa zao na kujiweka mbele katika Serikali. Utawaona mahali Serikali ipo wanajiingiza pale wakisema kwamba wao wanaomba lakini wanajificha ili matendo yao ya kinyama na kishetani yasijulikane. Mimi ni Mkatoliki na ninataka kushukuru Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki kwa kusema kwamba muda umefika wa kutunga sheria ya kuangalia makanisa yanayotumika. Kule kwangu kuna watu wanajiita waombezi ambao wameharibu familia nyingi za watu. Anaweza kuja aseme bibi yako anakuroga ama kuna mtu wako mchawi. Familia zinakosana. Ni vipi binadamu wa kawaida anaweza kuuza mali yake yote? Umesikia mtu aliuza mali yake akapata milioni 50 akampelekea pastor kisha akaenda msituni kuomba ili afe. Hili ni jambo ambalo linataka kuchunguzwa. Tunajiuliza maswali mengi ambayo hayana majibu. Huyu pastor mhalifu alipataje ekari 800 ikiwa Serikali haijui matendo yake? Mimi hata sijafikisha ekari tatu za shamba lakini yeye ana ekari 800 ambapo anazika watu ndani ya msitu na watu hawajui. Tunataka mienendo ya wahubiri ichunguzwe. Itikadi zao kali zimeleta maafa katika nchi hii. Nasikia kuna Yesu amepatikana Tongaren. Huyo yesu asiposimamishwa saa hii, tutapata maafa kama haya ya Mhubiri Mackenzie tunayoyazungumzia. Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa muda."
}