GET /api/v0.1/hansard/entries/1236311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236311,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236311/?format=api",
    "text_counter": 389,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia. Kwanza, kwa niaba yangu na niaba ya watu wa Jomvu, nachukua fursa hii kutoa rambirambi zangu kwa watu wa Malindi kwa yale maafa yametokea. Pili, ninampongeza Mhe. Owen Baya kwa kuleta hili jambo. Kama halingekuwa yeye kuleta hili jambo, hatungeweza kulizungumzia. Nasema kitu kimoja kumhusu Pastor Mackenzie. Hata sijui twaongea stori nyingi za nini kwa sababu ameleta maafa zaidi ya watu 100. Nilipofanya uchunguzi wangu, nasikia alikuja Malindi mwaka wa 2003. Hatujui kutoka siku hiyo hadi wa leo ni watu wangapi ameweza kuua. Yawezekana kuwa ni zaidi ya 500, 600 au hata 700. Kwa hivyo, huyo mtu hafai kuzunguka dunia hii. Ninataka kuzungumzia kuhusu watu kufuata dini sawasawa kwa sababu Matayo 7:7 yasema: “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango.” Ninataka kuongea maneno haya nikinukuu Biblia. Hawa wangelikuwa wanafuata Bibilia sawasawa, hawangeweza kudanganywa wafunge mpaka wajiue wenyewe. Jambo lingine la muhimu ni kwamba katika Idara ya Ujasusi, kuna kitengo ambacho kinashughulikia mambo ya trade unions, wanasiasa, kitengo kinachoshughulikia mambo ya dini ambacho wakati wa nyuma watu walikuwa wakipeleka taarifa katika Idara ya Upelelezi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}