GET /api/v0.1/hansard/entries/1236312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236312,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236312/?format=api",
"text_counter": 390,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "kule Mombasa na watu wakafuatwa mpaka Msikiti Musa. Vitengo hivi vyote vimelala. Kile kitengo ambacho chafanya kazi zaidi ni hiki cha kufuata wanasiasa. Vitengo vya ujasusi vyatakikana vijue wafanyibiashara wanafanya nini, waumini wanaoomba wanafanya mambo gani na mambo yote yanayotokea katika nchi. Sikubaliani kusema eti ekari ilikuwa 800 kwa hivyo ni msitu mkubwa hawakujua watu wanafanya nini. Serikali hata msitu uwe ekari 8000, ni muhimu ijue kila doti ya mahali ya nchi. Ukienda kule Lamu, kuna mahali panaitwa Majlis. Ni hoteli nzuri sana. Kuna mzungu mmoja, raia wa Ufaransa, ambaye alikuwa mlemavu. Alipotekwa nyara na kupelekwa Somalia, alisababisha Jeshi la Amerika kuingia Somalia kufuata mtu wao. Kwa hivyo, kutokana na vifo vya watu takriban 100, huyu mchungaji Mackenzie hastahili kabisa kuwa anazunguka na kupewa dhamana ya shilingi 100,000. Jambo hili linatamausha kwa sababu amefanya kosa hilo. Ningependa kuiomba Serikali iende kule na nguvu ndio jambo kama hili lisiweze kutokea tena. Ninaungana na wenzangu kuhusu huyu ‘Yesu wa Tongaren.’ Mimi ninavyofahamu, Yesu hakuoa. Lakini huyu ‘Yesu wa Tongaren’ ana wake wanne. Kwa hivyo, inafaa tumzuie kabla pia yeye hajatuletea maafa. Ni juzi tu huyu ‘Yesu wa Tongaren’ alitaka kusulubiwa na akakimbilia polisi. Tunafaa kumsimamisha kabla hajatuletea maafa kama ya Kilifi. ‘Yesu wa Tongaren’ akae atulie na bibi zake, na watu waende makanisani kufanya maombi. Nawapa pole watu wa Malindi. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}