GET /api/v0.1/hansard/entries/1236314/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236314,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236314/?format=api",
"text_counter": 392,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninaanza kwa kusema: Inaa Lillahi Wa Inna Ilayhi Raji’un (We belong to Allah and to Him we shall return). Ninasema pia pole sana kwa watu wa Kilifi na Kenya kwa jumla kwa msiba mkubwa kama huu. Waswahili wanasema: “Usipoziba ufa, utajenga ukuta.” Waziri alipoliangazia suala hili, kama tu Serikali ingetilia maanani na kuangalia njia ya kuzuia jambo hili, leo tusingekuwa tunazungumzia maafa ya zaidi ya watu 90 katika nchi yetu ya Kenya. Ni lazima tuangalie zile nyumba ambazo ni za ibada. Zimekuja nyingi sana na zina majina tofauti tofauti. Mhe. Alice amezungumzia wakili Magu ambaye aliua mke wake na kumchoma, kuua watoto wake na kisha kujiua yeye mwenyewe. Hii ni baada ya kuingizwa katika kanisa na mhubiri mmoja aliyefahamika kama Anne Wanjiru. Kwa hivyo, tunapozungumzia suala hili, ni muhimu tujue hivi sasa tuna madhehebu mengi. Tukubali kama Wakenya kuwa jambo ambalo linazungumziwa la illuminati limeingia sana katika taifa letu. Watu wanaingizwa katika mambo ya kishetani wakitumia jina la dini ambalo si kweli. Juzi tumeona mwanamke aliyemkatakata mtoto wake kwa kumdunga kisu na kisha kula viungo vyake vya ndani. Mambo hayo hayakuwahi kufanyika hapo zamani. Ila, lazima tujiulize; tuko wapi? Kama viongozi, ni lazima tuwakaribie wapiga kura. Iwapo Mhe. Owen na Waheshimiwa wengine wa Kilifi wangekuwa karibu na kuwatembelea watu wao waliowapigia kura kila mara, basi jambo hili lingekuwa limejulikana haraka. Haiwezekani maiti zaidi ya 200 ziweze kuzikwa ilhali kuna vijana ambao wanawekwa kama walinzi wa kuchunga watu wasitoroke na jambo lisijulikane. Hakuna siri ya watu wawili. Ikizidi tu watu wawili, basi hiyo si siri tena. Lazima itajulikana. Ni masikitiko makubwa. Tunajiuliza maisha ya Mkenya yako wapi? Wakati tunasema kuna uhuru wa kuabudu, ni lazima tujue pia kuna haki ya Mkenya ya kuishi. Haki ya Mkenya ya kuishi lazima ilindwe na kuchungwa. Hakuna uhuru ambao hauna kizuizi. Uhuru wowote lazima uwe na kizuizi. Huwezi kuwa na uhuru wa kuabudu katika hali ya kuhujumu wananchi wengine katika maafa kama haya. Ni masikitiko makubwa sana. Zaidi, huyu mchungaji Mackenzie akiwa kortini alisema: “Hamjui mnachopigana nacho, kitawaramba!” Matamshi hayo yanatuambia kwamba huyu hayuko peke yake. Lazima The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}